Posts

Showing posts from January, 2018

TUBUNI UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA

Image
Ipo siri kubwa katika Ufalme wa Mungu. Siri ya Ufalme wa Mungu anaijua Mungu mwenyewe. Hutufunulia yeye mwenyewe inavyompendeza. Hotuba ya kwanza ya mlimani Yesu alianza kuhubiri habari za Ufalme wa Mungu. Alitufundisha jinsi ya kuurithi Ufalme wa Mungu pia, aina ya watu wanaostahili na alitaja makundi mbalimbali kwa kusema. “Heri wenye moyo safi maana hao watamwona MUNGU” Mathayo 5:8. -         Wale wanaojishusha na kumtafuta Mungu kwa bidii, kwa unyenyekevu na uvumilivu, wana heri kwa sababu hatimaye wataurithi Ufalme wa Mbinguni. -         Kila alipokwenda aliwaambia, “Tubuni ufalme wa Mbinguni umekaribia”. Waliotubu walipita na wapo Mbinguni. -         Yohana naye alifundisha na kusema “Tubuni Ufalme wa Mungu umekaribia” na kumtengenezea Yesu njia. Waliotubu walipita na wapo Mbinguni. Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na ...