TUBUNI UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA
Ipo siri kubwa katika Ufalme
wa Mungu. Siri ya Ufalme wa Mungu anaijua Mungu mwenyewe. Hutufunulia yeye
mwenyewe inavyompendeza. Hotuba ya kwanza ya mlimani Yesu alianza kuhubiri
habari za Ufalme wa Mungu. Alitufundisha jinsi ya kuurithi Ufalme wa Mungu pia,
aina ya watu wanaostahili na alitaja makundi mbalimbali kwa kusema.
“Heri
wenye moyo safi
maana hao watamwona MUNGU” Mathayo 5:8.
-
Wale
wanaojishusha na kumtafuta Mungu kwa bidii, kwa unyenyekevu na uvumilivu, wana
heri kwa sababu hatimaye wataurithi Ufalme wa Mbinguni.
-
Kila alipokwenda
aliwaambia, “Tubuni ufalme wa Mbinguni umekaribia”. Waliotubu walipita na
wapo Mbinguni.
-
Yohana naye
alifundisha na kusema “Tubuni Ufalme wa Mungu umekaribia” na kumtengenezea Yesu
njia. Waliotubu walipita na wapo Mbinguni. Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji
akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, tubuni maana Ufalme wa Mbinguni
umekaribia. Mathayo 3:1-2
Yesu aliwaambia mitume na
wafuasi wake; kila mtakapofika hubirini Ufalme wa Mungu, semeni hivi “Tubuni
Ufalme wa Mbinguni umekaribia”. Nao waliotubu walipita wakaenda
mbinguni.
Tokea wakati huo Yesu alianza kuhuiri, na kusema, Tubuni kwa maana
ufalme wa Mbinguni umekaribia Mathayo 4:17
Katika hotuba alizozifanya
Mlimani alikuwa akizungumzia na kukazia kuhubiri Ufalme wa Mbinguni na
alihubiri siri nyingi za Ufalme wa Mbinguni.
Katika Mathayo 24:1-51. Yesu alizungumzia kuhusu siku za
mwisho. Wanafunzi wake walipata hofu sana
na kujiuliza kuhusu dalili za kurudi kwake. Baada ya kupaa kwake tazama wale wanafunzi
waliendelea kuhubiri Ufalme wa Mungu. Watu wengi waliendelea kutubu na wakapita
na wapo Mbinguni baada ya wale wanafunzi kuondoka duniani wengine waliendelea
kuhubiri habari za Ufalme wa Mbinguni hadi sasa. Watu wengine walipotubu
walipita na wapo Mbinguni. Mbingu bado haijajaa, Bwana Yesu alisema. “Mbinguni
kwa baba yangu kuna makao mengi. Yohana 14:2.
Kuna wahubiri wengi
wanadanganya watu kwamba Mbinguni kumeshajaa. Ingekuwa kweli Bwana Yesu
asingetupa moyo ila angesema kuna kipindi mbingu zitajaa.
Injili iliendelea kuhubiriwa
ikikazia watu watubu ili waweze kwenda Mbinguni hadi sasa na wengi wanapita na
wanaendelea kupita. Hili Neno Ufalme wa Mbingu Umekaribia, ni Neno lenye
siri kubwa kwa sababu kila linapohubiriwa watu wanaliona jipya kila siku. Na
Yesu anaendelea kuvuna watu kwa mahubiri ya Neno hili “Tubuni Ufalme wa Mbinguni
umekaribia”.
Yesu anakaribia kurudi.
Sasa imefikia kwamba mavuno yanavunwa kwa wingi kwa sababu
Ufalme wa Mbingu umekaribia kwelikweli (sana)
katika Mathayo 24 na Isaya 24 Yesu alieleza mambo yatakayotokea siku za mwisho
wakati atakapokaribia sana
kurudi. (Haya maneno aliyoyasema kuhusu kurudi kwake na ishara zitakazoashiria
kurudi kwake). Alisema alipokuwa haa duniani katika Mathayo 24 na alipokuwa
Minguni alinena kwa kutumia kinywa cha Nabii Isaya katika sura 24. ndiyo mambo
ambayo yalishaanza na yanaendelea kutokea na karibu sana yatafika ukingoni.
Sasa hii Neno “Tubuni
Ufalme wa Mbinguni umekaribia” ni Neno ambalo linatakiwa lihubiriwe kwa
nguvu ili kuvuna wateule wengi kwa ajili ya kuvutwa pale mawinguni.
Comments
Post a Comment